Numbers 15:4-9
4 andipo yeye aletaye sadaka yake ataiweka mbele za Bwana sadaka ya nafaka, sehemu ya kumi ya efa ▼▼ Sehemu ya kumi ya efa ni sawa na kilo moja.
ya unga laini uliochanganywa na robo ya hini ▼▼ Robo ya hini ni sawa na lita moja.
ya mafuta. 5 dPamoja na kila mwana-kondoo kwa ajili ya sadaka ya kuteketezwa au dhabihu, andaa robo ya hini ya divai kwa sadaka ya kinywaji. 6 e“ ‘Pamoja na kondoo dume andaa sadaka ya nafaka ya sehemu mbili za kumi za efa ▼▼ Sehemu mbili za kumi za efa ni sawa na kilo 2.
za unga laini uliochanganywa na theluthi moja ▼▼ Theluthi moja ya hini ni sawa na lita moja na nusu.
ya hini ya mafuta, 7 hna theluthi moja ya hini ya divai kama sadaka ya kinywaji. Vitoe kama harufu nzuri inayompendeza Bwana. 8 i“ ‘Unapoandaa fahali mchanga kama sadaka ya kuteketezwa au dhabihu, kwa ajili ya nadhiri maalum au sadaka ya amani kwa Bwana, 9 jleta pamoja na huyo fahali sadaka ya nafaka ya unga laini sehemu tatu za kumi za efa ▼▼ Sehemu tatu za kumi za efa ni sawa na kilo 3.
uliochanganywa na nusu ya hini ▼▼ Nusu ya hini ni sawa na lita 2.
ya mafuta.
Copyright information for
SwhKC